SHERIA2
Don't miss

Sunday, July 7, 2013

AJIRA HATARISHI KWA WATOTO NA SHERIA TANZANIA


By on 2:42 PM



Kitabu hiki hapa juu cha Sheria kwa Kiswahili, pamoja na mambo mengine, kimeelezea juu ya marufuku ya ajira hatarishi kwa watoto. Sheria ya Watoto Namba 21 ya 2009 pamoja na Sheria ya Ajira na mahusiano kazini hapa Tanzania, zinaeleza kuwa, ni marufuku kwa mtu yeyote kumfanyisha mtoto kazi hatarishi au zile zinazovurugha maslahi yake bora.

Mtoto ni nani? Mtoto ni mtu yeyote aliyepo chini ya miaka 18. pamoja na kwamba inaruhusiwa kumwajiri mtoto wa miaka chini ya 18 lakini si chini ya 14 kwa kazi nyepesi tu au zile zinazohusisha mafunzo, ni marufuku mtoto huyo kufanya kazi za usiku wa kuanzia saa mbili usiku na kuendelea. Inaelekeza kuwa, mtoto ana haki ya kufanya kazi, lakini zile zinazohatarisha ustawi bora wa mtoto kama vile kazi za viwandani, migodini, magari ya masafa marefu, kwenye meli, kwenye kemikali, baa na kumbi za starehe na maeneo yanayoweza kuharibu tabia yake n.k ni marufuku. hata hivyo, kazi za melini na migodini, viwandani n.k kama atakuwa anafanya kama moja ya mafunzo yake, pengine  ni mwanafunzi na anafanya mafunzo kwa vitendo, inaruhusiwa; isipokuwa, sheria inataka uangalizi wa karibu kabisa wa mtoto huyo aliyepo mafunzoni uwepo. ni marufuku kumfanyisha mtoto au kumweka katika mazingira yatakayohatarisha ustawi bora wa mtoti, iwe kiafya, kielimu, kitabia n.k

hapa Tanzania wapo watoto wengi tu wanafanya kazi migodini, kwenye mabaa na kumbi za starehe. ukisoma kitabu hicho hapo juu utajua haya yote. kwa Arusha kinapatikana KASE Stores Bomani street karibu ELCT building, Dar es salaam fika imalaseko supermarket posta na bookshop karibia zote kubwa. mwanza fika serengeti bookshop, victoria bookshop, Bookpoint bookshop na Gunda bookshop. kahaa utakipata pale royal supermarket na stationaries stand kuu ya mabasi, moshi utapata bookshop zote za pale mjini, iringa na mbeya kitafika mwezi ujao. kwa mawasiliano zaidi piga 0767 154141. karibuni sana.

About Syed Faizan Ali

Faizan is a 17 year old young guy who is blessed with the art of Blogging,He love to Blog day in and day out,He is a Website Designer and a Certified Graphics Designer.

0 comments:

Post a Comment